Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro anawatangazia Wananchi wote wenye sifa kutuma maombi ya kazi kwa kuzingatia vigezo na maelekezo yaliyo katika tangazo hili. Nafasi zinazotangazwa ni:-
1. Mtendaji wa Kijiji daraja la III (Nafasi 23)
Sifa za Mwombaji
Awe na Elimu ya Kidato cha nne (IV) au sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya (Cheti) Astashahada (NTA LEVEL 5) katika mojawapo ya fani zifuatazo:- Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote kinachotambulika na Serikali.
Ngazi ya Mshahara
Kwa kuzingatia viwango vya mishahara vya Serikali ngazi ya Mshahara ya TGS B (Tsh. 390,000/=) kwa mwezi.
Kazi za kufanya
2. Katibu Mahsusi daraja la III (Personal Secretary III) nafasi (01)
SIFA
Awe na Elimu ya kidato cha nne (iv) aliyehudhuria mafunzo ya uhazili na kufaulu mtihani wa hatua ya tatu, awe amefaulu somo la hati mikato ya kiswahili na kiingereza maneno 80 kwa dakika moja na awe amepata mafunzo ya Compyuta kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na kupata cheti katika programu za Window Microsotf Office, Internet, Email na Publisher.
Ngazi ya Mshahara
Kwa kuzingatia viwango vya mishahara vya Serikali ngazi ya Mshahara ya TGS B (Tsh. 390,000/=) kwa mwezi.
Kazi za kufanya
Vigezo na masharti ya jumla kwa waombaji
JINSI YA KUTUMA MAOMBI
Barua zote ziwe na anuani ya mwombaji na namba ya simu (kama ipo) na zitumwe kwa:-
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro,
S.L.P. 1,
LOLIONDO.
Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 11/09/2017 saa tisa na nusu (9:30) alasiri.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.