Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Ngorongoro bwana Raphael John Siumbu anawatangazia watumishi wote wa Umma katika Wilaya ya Ngorongoro kuwa zoezi la uhakiki katika mfumo wa LAWSON na NIDA katika tarafa ya Ngorongoro litafanyikia katika Halmashauri ya Wilaya ya Karatu kuanzia tarehe 10/07/2017. Zoezi hili ni kwa awamu ya Pili baada ya kukamilisha uhakiki katika Tarafa na Sale na Loliondo siku ya tarehe 08/07/2017.
Lengo la Kufanya uhakiki katika Eneo la jirani (Halmashauri ya Wilaya Karatu) ni kuweza kuwahakiki watumishi wa Tarafa ya Ngorongoro kwa urahisi ukizingatia umbali kutoka makao makuu ya Wilaya (Loliondo). Hivyo basi watumishi wote wa Umma wa Wilaya ya Ngorongoro mnakaribishwa katika Halmashauri ya Karatu Mkiwa na nakala ya Hati ya Malipo ya Mshahara (salary Slip), Kitambulisho cha NIDA na Kitambulisho cha Mfanyakazi.
Zoezi hili litafanyika kwa muda wa siku nne yaani kuanzia tarehe 10/07/2017 hadi tarehe 13/07/2017 hivyo basi mnaombwa kuwahi ili kuweza kuhakikiwa kwa wakati.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.