Mkutano Mkuu wa Kijiji ni chombo cha utawala kinachoundwa na wajumbe wafuatao:-
• Wakazi wote wa Kijiji wenye umri usiopungua miaka 18 na wenye akili timamu;
• Mwenyekiti wa Kijiji;
• Wenyeviti wa Vitongoji vyote kijijini;
• Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji ambao ni kati ya 15 na 25;
• Afisa Mtendaji wa Kijiji – Katibu.
Muundo wa Kamati za Halmashauri ya Kijiji
Halmashauri ya Kijiji inapaswa kuunda kamati zifuatazo:-
1. Kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango;
2. Kamati ya Huduma za Jamii na shughuli za kujitegemea;
3. Kamati ya Ulinzi na Usalama.
Aidha, Halmashauri ya Kijiji inaweza kuunda kamati nyingine kwa kuzingatia mahitaji na vipaumbele vya kijiji.
Muhimu: Kamati zote za kudumu za Halmashauri ya Kijiji zinatakiwa kukutana kabla ya kila mkutano wa Halmashauri ya Kijiji, ili kila Kamati iweze kutoa taarifa yake katika mkutano huo wa Halmashauri ya Kijiji.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.