NGORONGORO ,ARUSHA
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Bw.Raphael J. Siumbu amewataka wakuu wa shule za sekondari kutambua na kutii mamlaka ya Maafisa Elimu Kata.
Bw.Siumbu ameyasema hayo jana tarehe 29 January 2019 wakati akihutubia mkutano wa mafunzo wa mfumo wa wazi wa utendaji (OPRAS) kwa wakuu wa shule za sekondari pamoja na Maafisa Elimu kata iliyofanyika katika Ukumbi wa shule ya Sekondari Loliondo
Akihutubia mkutano huo uliowakutanisha Wakuu wa shule za sekondari kutoka Tarafa ya Sale na Loliondo Siumbu amebainisha kuwa Maafisa Elimu kata ndio waakilishi wa ngazi za juu za serikali kwenye kata zao na hivyo kuwataka wakuu wa shule kuheshimu mamlaka za Maafisa hao na kutoa ushirikiano kikamilifu.
Pamoja na Hayo Bwana Siumbu vilevile ametoa wito kwa Maafisa Elimu kata na Wakuu wa shule kufuata sheria na maelekezo katika kusimamia majukumu waliyopewa pamoja na kuongeza kuwa changamoto zilizopo haziwezi kutatululiwa kwa wakati mmoja lakini akahahidi kuwa serikali itaendelea kutatua changamoto zilizopo
Imetolewa na,
Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro
Maafisa Elimu Kata na Wakuu wa shule wa Tarafa za Loliondo na Sale waliohudhuria Mafunzo ya Ujazaji wa Fomu za OPRAS wakiwa katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Loliondo
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Bw.Raphael J.Siumbu akifungua mafunzo ya ujazaji wa fomu za OPRAS katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Loliondo
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.