Karibu kwenye tovuti rasmi ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, katika tovuti hii utapata taarifa mbalimbali kuhusu majukumu ya Halmashauri ya Wilaya katika kuratibu na kusimamia huduma za kiuchumi na kijamii zinazotolewa. Pia utapata kujua muundo wa halmashauri na maeneo ya utawala ikiwa ni pamoja na majukumu ya idara na vitengo, machapicho mbalimbali, orodha ya Waheshimiwa madiwani na kata zao, miradi na fursa za uwekezaji. Aidha katika tovuti hii utapata kufahamu taratibu mbalimbali unazotakiwa kufuata ili kupata huduma kwenye Halmashauri. Pia miongozo na nyaraka mbalimbali zipo kwenye tovuti hii. Ukiwa Mdau wa maendeleo tunategemea ushauri wako katika kuleta maendeleo kwa wananchi wetu. Ni Matumaini yangu kuwa utatembelea tovuti hii mara kwa mara ili kufahamu jinsi Halmashauri inavyotekeleza majukumu yake na kupata taarifa ya matukio mbalimbali.
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro tunaamini katika Uwazi, Uwajibikaji na Ushirikiano katika kuelekea Maendeleo Endelevu.