Mhe. Shutuk Kitamwas, Diwani wa kata ya Alailelai anawakaribisha ndugu jamaa na marafiki wa Kata ya Alailelai katika harambee ya kujenga mabweni ya shule ya msingi Alailelai. Harambee hiyo itafanyika siku ya jumamosi tarehe 14.04.2018 katika Shule ya Msingi Alailelai kuanzia saa 3:00 Asubuhi hadi saa 10:00 Jioni.
Katika kufanikisha shughuli hii muhimu Mhe. Kitamwas na kamati nzima ya ujenzi wa mabweni hayo anapokea michango mbalimbali ikiwa ni pamoja na saruji ‘cement’, mabati, mbao, misumari na vyote vinavyoweza kufanikisha kazi hiyo. Aidha kutokana na majukumu na umbali, kwa wale wote wasioweza kufika katika harambee hiyo, Mhe. Kitamwas anaomba wafanye mawasiliano kupitia namba +255764039093 au +255689109096 ikiwa ni pamoja na kutuma michango yao katika kufanikisha jambo hili jema.
Elimu ni Ufunguo wa Maisha, Tuijenge Ngorongoro yetu.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.