Kitengo cha Ugavi ni moja wapo ya vitengo vilivyo chini ya Ofisi ya Mkurugenzi katika Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro.
Majukumu makubwa ya Kitengo hiki ni kama ifuatavyo;
kutekeleza Sheria mpya ya Manunuzi Na. 7 ya mwaka 2011, na Kanuni ya Manunuzi Na. 446 ya mwaka 2013 na kuhakikisha kuwa manunuzi hayo yanafuata na kuzingatia Sheria na Kanuni hizo.
Kitengo kinatoa ushauri kwa Idara na Vitengo kufuata Mpango wa Manunuzi.