Baraza la Halmashauri Wilaya ya Ngorongoro likiongozwa na mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Manja Sirongo diwani wa kata ya Soitsambu limezitambua shule, wadau wa maendeleo na vjjiji vilivyofanya vizuri kuchangia maendeleo sekta ya elimu wilayani na kutumia fursa hiyo kutoa zawadi ya vyeti na fedha ikiwa ni sehemu ya motisha na kutambua juhudi zinazofanywa na makundi hayo kuhakikisha jamii ya Ngorongoro inasonga mbele katika nyanja tofauti.

Katika Baraza hilo limetoa zawadi kwa shule zote za Msingi na Sekondari zilizofanya vizuri kwenye mitihani ya Taifa na kupongeza wadau wa sekta ya elimu walitoa mchango mkubwa kwa sekta ya elimu kukua.
Shule za msingi na sekondari zilizofanya vizuri katika mitihani ya kitaifa iliyofanyika mwaka 2025 ni pamoja shule ya msingi Bulati imeongoza matokeo ya darasa la saba, shule ya msingi Endulen, Soitsambu kwa shule za Serikali kwa shule za binafsi shule ya msingi Lumo, Bright na Butemine na mtihani wa darasa la nne ni shule ya Indoinyo, Mama Sylvia na Alailelai kwa shule za Serikali huku shule binafsi zikiongozwa na St luke, Bright pamoja Butemine.

Aidha shule za Sekondari zilizofanya vizuri kidato cha nne ni shule ya sekondari Emanyata Ngorongoro girls asilimia, Loliondo sekondari, Samunge Sekondari na Malambo Sekondari.
Matokeo ya shule za Sekondari zilizofanya vizuri kidato cha sita ni Digodigo, Embarway na Nainokanoka zimefaulisha kwa asilimia 100 zikifuatiwa na Loliondo sekondari asilimia 99, Samunge asilimia 98.8 na Malambo asilimia 96.9.

Pia, Mashirika ya KFW, THOMSON safaris, PWC na padre Fredrick wa Kijiji cha Maalon pamoja na wananchi wa Kijiji cha Oldonyosambu wote hawa wametambuliwa na Baraza kwa kusaidia kuinua sekta ya elimu wilayani Ngorongoro.

Pongezi hizo zimetolewa tarehe 20 Februari, 2026 wakati wa mkutano wa kikao cha Baraza la Halmashauri kipindi cha robo ya pili kilichofanyika katika ukumbi wa wa mkutano wa Halmashauri.

https://www.instagram.com/reel/DU_bwsCDCP5/?igsh=ODIxbXFnamY4M3h6
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.