Baraza la wafanyakazi Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro limepitia, limejadili na kupitisha rasimu ya mpango wa bajeti itakayotekelezwa mwaka wa fedha 2026/2027. Rasimu hiyo imewasilishwa na Afisa Mipango wa Halmashauri Bi. Emmy Hongori

Mkutano wa Kikao hicho kimeongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Bw. Murtallah S. Mbillu leo tarehe 13 Februari, 2026 katika ukumbi wa Mkutano, pamoja na kupokea rasimu hiyo Mkurugenzi ametoa nafasi kwa wajumbe ambapo wametoa maoni yatayokwenda kusaidia katika uboreshaji wa bajeti kwa maslahi mapana na maendeleo ya Halmashauri na wafanyakazi.

Aidha, Baraza limejadili bajeti inayoendelea kutekelezwa ya mwaka wa fedha 2025/2026. Pia changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi katika kutekeleza majukumu yao zimejadiliwa na kutoa ushauri namna ya kuzikabili changamoto hizo ili kuongeza ufanisi kazini.

Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.