Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro imenunua jumla ya dozi 44,000 za chanjo kwaajili ya kuchanja mbuzi na kondoo ili kudhibiti ugonjwa wa homa ya mapafu (CPPP) kutoka kwa Wakala wa Maabara ya Vetenari Tanzania Kanda ya Kaskazini (TVLA).
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Murtallah Mbillu, amesema Halmashauri imepokea jumla ya dozi 2,000 za chanjo ya Homa ya Mapafu ya Mbuzi (CPPP) kutoka Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania. Lengo la serikali ni kuimarisha afya za mifugo na kuboresha uchumi wa wananchi wa Ngorongoro, ambao asilimia 80 ni wafugaji huku Wilaya hiyo ikiwa na mifugo mingi zaidi
Naye Kaimu Meneja wa Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania Kanda ya Kaskazini (TVLA) Dk,Lowenya Mushi, amesema kuwa lengo la ni kuhamasisha wananchi kuchanja mifugo yao ili kutokomeza kabisa ugonjwa huo ambao umekuwa changamoto kwa muda mrefu.
Diwani wa Kata ya Oloipiri, Lucas Krusas, ametua nafasi hiyo kuishukuru Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi za kudhibiti ugonjwa wa homa ya mapafu kwa mifugo kwani ni hatua muhimu kwa wafugaji.
Pia, amewahimiza wananchi kujitokeza kuchanja mifugo yao ili kuboresha afya ya mifugo na kuinua hali ya uchumi kwani hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa serikali kuhakikisha mifugo inakuwa na afya bora, hali inayotarajiwa kuchochea ustawi wa jamii za wafugaji katika Wilaya ya Ngorongoro.
Mmoja kati ya wananchi walionufaika na uchanjaji wa mifugo hiyo katika kijiji cha Oloipiri, Lucas Morijo ametoa shukrani kwa Halmashauri na TVLA kuchanja mifugo yao kwani ugonjwa huo umekuwa tishio kwa mifugo na kudidimiza uchumi wa wafugaji na kuiomba Serikali kuendelea kuchanja mifugo ili isishambuliwe na magonjwa.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.