Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Bw. Murtallah S. Mbillu leo tarehe 26 Septemba, 2024 ametoa maelekezo kuhusu utaratibu Kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba 2024.
Maelekezo yaliyotolewa na Msimamizi wa Uchaguzi ni pamoja na siku ya uchaguzi, muda na sehemu yakuandikishia wapiga Kura, muda na mahali pakufanyia uchaguzi , sifa za wananchi wenye sifa stahiki za kupiga kura na kugombea nafasi za uongozi, nafasi zinazogombewa, siku ya utoaji na urejeshwaji wa fomu za kugombea nafasi za Uongozi wa Serikali za Mitaa, uteuzi wa Viongozi, Ukataji wa rufaa, siku na utaratibu wa Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Aidha Bw. Murtallah ametoa wito kwa Wananchi kujitokeza katika kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Kwa kufuata kanuni na taratibu zilizotolewa ili kuhimiza maendeleo ya Jimbo na Taifa Kwa Ujumla.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.