Timu kutoka Wizara ya katiba na Sheria ikiongozwa na Wakili Joyce Mushi imeendelea na zoezi la kutoa mafunzo ya sheria na utawala Bora kwa viongozi wa Serikali za Mitaa wakiwemo Wakuu wa Divisheni, Watendaji wa Kata pamoja na Kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Ngorongoro.
MAFUNZO hayo yameangazia katika nyanja mbalimbali kama umuhimu wa Demokrasia, kuheshimu katiba, Sheria, haki za binadamu pamoja na umuhimu wa kufuata kanuni za utawala bora ili kuwafanya Wananchi kupata haki zao za kisheria pamoja na kupata maendeleo ikiwa na kutoa taarifa zote muhimu kwa wananchi ili kujenga na kuimarisha uhusiano kati ya Wananchi na Serikali.
Aidha, Bw. Yohana Mcharo amewataka Watumishi wa Umma kila mmoja kutimiza wajibu wao, huku akiwahasa kuitambua kila mmoja anatekeleza majukumu yake kwa kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo wanatakiwa kuzingatia Sheria na utaratibu ili kuwatumikia Wananchi vyema bila kuwanyanyasa.
Mafunzo hayo yametolewa Leo tarehe 18 Machi, 2025 katika ukumbi wa Halmashauri huku timu hiyo imekaribishwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bw. Bennezeth Bwikizo.
Hata hivyo Wakili Joyce Mushi ametumia fursa hiyo kutoa shukrani kwa uongozi wa Halmashauri na kuwakumbusha lengo la mafunzo haya ni kuusaidia uongozi kutekeleza miradi yote inayotekelezwa na Serikali kwa uadilifu mkubwa kuanzia ngazi ya kata ili Wananchi wote kunufaika na matunda ya maendeleo yanayotekelezwa na Serikali yao.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.