Wilaya ya Ngorongoro imenufaika na pikipiki Saba ( 7)zilizotolewa na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa watendaji wa kata ili kuwasaidia kuwahudumia wananchi kwa urahisi zaidi.
Hayo yameelezwa leo Feb 18, 2023 na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro Dkt. Juma Mhina katika kikao Kazi cha lishe kitaifa ngazi ya wilaya ambacho kimehusisha Ofisi ya mkuu wa Wilaya ,Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji na Maafisa Watendaji wa kata Wilayani hapa.
Ambapo amewasihi watendaji wote wa kata kusimamia udhibiti wa ukusanyaji wa mapato hasa katika minada,kusaidia maafisa biashara uhamasishaji wa ukataji leseni za biashara katika maeneo yao na kuwasimamia viongozi wengine katika kata na vijiji kama vile Mafisa elimu kata kwani wao ni wawakili wa Mkurugenzi katika kata.
Na kuhusiana na lishe amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa pikipiki NNE(4) ambazo zinasaidia kufikiwa wananchi na wataalam wa lishe hivyo kupelekea wilaya ya Ngorongoro kuwa wa kwanza katika Mkoa wa Arusha kwenye viashiria vya lishe hivyo amewataka watendaji kusimamia mikataba ya lishe katika maeneo yao ili kuinua zaidi hali ya lishe hasa kwa watoto akisisitiza kua mtoto asie na lishe bora hawezi kuwa na ukomavu wa uelewa yani akili .
"Kutokuhudhulia klinik katika miezi ya kwanza ya ujauzito na kutozingatia mlo kamili kwa watoto zimetajwa kama changamoto kubwa zinazosababisha uduumavu kwa watoto katika jamii" amesema Dkt Mhina
Afisa mtendaji kata ya kirangi ndugu Paulo Azael anasema watahakikisha wanatekeleza maelekezo yote waliyopewa ikiwemo ya kusimamia mikataba ya lishe,kwa upande wake Christina Agustino kaimu Afisa mtendaji kata ya Digodigo anasema ushiriki wa wanaume ni mdogo katika malezi hasa ya lishe kwa watoto.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.