Na Joseph K. Edward-NDC HABARI
Mhe. Paul Makonda amesema anatarajia kuanza ziara ya kutembelea Wilaya zote zilizopo mkoani Arusha ambapo katika kila Wilaya atatumia muda wa Siku mbili kusikiliza na kutatua kero za Wananchi wote watakaokua na matatizo mbalimbali ikiwemo wale waliodhulumiwa haki zao katika maeneo yote atakayopita.
Akizungumza katika Mkutano wake na Wananchi wa Mkoa wa Arusha leo tarehe 10 Mei, 2024, Mhe Makonda amesema kuwa atatumia muda wa Siku mbili kuwasikiliza Wananchi katika kila Wilaya .
"Kuanzia tarehe 20 Mungu akitupa uhai tutafanya Ziara ya kila Wiaya, kulingana na taarifa nilizonazo kuna watu wamekosa nauli, sasa kama wamekosa nauli Daktari Samia Suluhu Hassan ananilipa Mshahara, amenipa na gari ameweka na mafuta mimi nitawafuateni huko huko waliko"-amesema Makonda.
Wilaya ya Ngorongoro ni miongoni mwa Wilaya itakayo tembelewa na Mhe. Paul Christian Makonda.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.