Jumla ya Wanafunzi 1840 wa kidato Cha nne Wilaya ya Ngorongoro wanatarajia kufanya mtihani wa Taifa wa elimu ya upili unaotarajiwa kufanyika jumatatu ya tarehe 11 Novemba 2024.
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro ina jumla ya shule 13 za Sekondari zenye idadi ya Watahiniwa 1840 kwa ujumla wake ambapo Watahiniwa 965 ni wavulana na Watahiniwa 875 ni wasichana.
Afisa Elimu Sekondari Mwl. Emmanuel Sukums amesema divisheni ya elimu imejipanga vizuri kwa muda wote wa kuanza kwa zoezi hili la mtihani mpaka litakapomalizika Pia, amewatakiwa maandalizi mema watahiniwa wote wilayani hapa.
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji Bw. Murtallah S. Mbillu kwa niaba ya uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro anawatakia kila la kheri na maandalizi mema Watahiniwa wote wa kidato cha nne wote wa mwaka 2024 hapa nchini.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.