• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhamira
    • Misingi mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Utumishi
      • Usafi na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Vijana
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji na Kilimo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba za Vikao
    • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Kata
      • Loliondo
        • Ololosokwan
        • Soitsambu
        • Enguserosambu
        • Maalon
        • Oloirien Magaiduru
        • Piyaya
        • Orgosorok
        • Oloipir
        • Arash
      • Ngorongoro
        • Alailelai
        • Naiyobi
        • Olbalbal
        • Nainokanoka
        • Kakesio
        • Ngorongoro
        • Eyasi
        • Endulen
        • Ngoile
        • Alaitolei
        • Misigyo
      • Sale
        • Sale
        • Malambo
        • Digodigo
        • Oldonyosambu
        • Samunge
        • Pinyinyi
        • Kirangi
        • Engaresero
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezw
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Majarida mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi

WANANCHI DIGODIGO NA SAMUNGE WAMEMSHUKURU MKUU WA WILAYA KUWATEMBELEA NA KUSIKILIZA KERO ZAO.

Posted on: March 14th, 2024


Wananchi Kata ya Samunge na Kata ya Digodigo leo Machi 14, 2024 wamemshukuru Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Kanali Wilson Sakulo kwa ziara yake ya kuwatembelea, kusikiliza na kutatua kero. Pia wamejitokeza kwa wingi ili kumsikiliza na kutoa kero zao katika Mkutano wa hadhara uliotishwa na Mkuu wa Wilaya  kisha kuonyesha kuvutiwa na njia hiyo aliyotumia Mhe. Mkuu wa Wilaya ya kuwasikiliza wananchi wake.


"Kwanza naipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutuletea miradi mingi, kwa kipindi cha miaka mitatu tumeletewa miradi yenye thamani ya bilion 1.2, ikiwemo Barabara, Shule pamoja na mradi wa umwagiliaji pia kwa kutuletea Mkuu wa Wilaya unayejali watu unaowaongoza  tunashukuru sana"-Mhe. Baraka Diwani wa Digodigo


Akizungumza katika Mkutano huo Bi. Beti Meriedi Mkazi wa Kijiji cha Mdito kata ya Samunge amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa ujio wake na kuitisha Mkutano ili Wananchi wenye kero na matatizo wapate msaada, amesema jambo hilo linawatia faraja.


" Mhe. Mkuu wa Wilaya tunashukuru kwa ujio wako ili wenye matatizo na wenye kero wapate msaada tunakushukuru sana na karibu Samunge"-Bi. Beti Meried


Hata hivyo wakati wa hotuba yake Mhe. Kanali Wilson Sakulo ametoa rai kwa Wananchi wa Digodigo na Samunge kutanua fikra zao katika upande wa maendeleo kwa kukubali wawekezaji wanapojitojeza katika maeneo yao kwaajili uwekezaji, kwani ndio chachu ya maendeleo ya Kata zao na Taifa kwa ujumla.


Mhe. Kanali Sakulo ameongeza kwa kusema kuwa Soko jipya la Wasso limeanza kutumika kwa shughuli za kuhudumia jamii katika upande wa mahitaji muhimu kama vyakula na nguo ambapo sehemu ya mnada kuanzia ijumaa ya tarehe 15 Machi utakua katika viunga vya Soko jipya hivyo wasisite kwenda kufanya biashara zao pale, kwa maana maeneo yapo ya kutosha na kila mfanyabiashara atapata eneo bila shida.


" Kuanzia kesho mnada wa mbogamboga, nguo na mahitaji yote isipokuwa mifugo utafanyikia katika viunga vya Soko jipya la Wasso na mnada wa zamani utabaki kama mnada wa mifugo tu, kwahiyo karibu sana miundo mbinu yote iko sawa na hakuna wa kuwasumbua" amesema Mhe. Kanali Sakulo.


Aidha Mkuu wa Wilaya ametoa agizo kwa Uongozi wa Kata ya  Digodigo watenge eneo maalumu kwaajili ya Soko kwa watu wa Digodigo amesema hayo wakati anajibu kero ya Wananchi wa Digodigo ya kutokua na sehemu maalumu ya Soko.


"Lazima tuwe na eneo la Soko hapa Digodigo na Watu waache hivyo nikirudi hapa nataka nikute Wananchi wamepata Soko la linatumika"ameongeza Kanali Sakulo


Kwa upande wakeKaimu Mkurugenzi wa TAKUKURU Bw. Kairo Mwafula ametoa elimu kwa Wananchi hao kupinga na kuzikataa njia za rushwa na kutoa taarifa pindi wanaposhuhudia au kuombwa rushwa na mtumishi yoyote wa umma kisha kutoa namba zake za simu ili pindi tukio lolote la rushwa linapotokea waweze kutoa taarifa haraka.


"Mapambano dhidi ya rushwa niyakwetu wote, uonapo vitendo vya rushwa toa taarifa kwenye Ofisi yoyote ya Umma au kwenye Uongozi wa kata, kijiji au Ofisi ya Mkurugenzi sisi tutalishughulikia, na hata ukiona TAKUKURU awawajibiki ipasavyo msisite kusema fikikenk Ofisini, piga simu au tuma ujumbe wa maandishi sisi tutalishughulikia wote waliyohusika"


Wakati wa Mkutano huo Mkuu wa Polisi Wilaya ya Ngorongoro Alphonce Bandia ametumia fursa kuwaasa Wananchi wanatumia vyombo vya moto kuwa na leseni, na wanaomiliki vyombo hivyo vya moto wahakikishe wanaajiri watu wenye taaluma ya udereva na wanaomiliki leseni ili kupunguza ajali na matatizo yanayouokea barabarani.


"Wewe unaendesha chombo cha usafiri cha moto hakikisha unamiliki leseni inayokuruhusu kuendesha hicho chombo mkifanya hivyo mtakua salama"-OCD Bandia


Ikumbukwe Kanali Wilson Sakulo, amekua na ziara ya siku tatu ya kufanya Mkutano wa hadhara ili kusikiliza na kutatua changamoto za Wananchi wa Ngorongoro, ambapo ameamua kuambatana na vyombo usalama, Taasisi mbalimbali kama TARURA, TANESCO, RUWASA, TAKUKURU pamoja na Wataalamu wa kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro ili kuhakikisha changamoto yoyote inayoyolewa na Wananchi utatuzi unalatikana.Pia ziara hiyo imeanza siku ya jumatano ya tarehe 13 Machi 2024 na inatarajia kumalizika siku ya kesho ijumaa ya tarehe 15 Machi 2024.


Kazi inaendelea...

Matangazo

  • TANGAZO LA RATIBA YA UCHAGUZI NA UANDIKISHAJI WA UCHAGUZI. September 26, 2024
  • TANGAZO LA UANDIKISHAJI VIJANA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA. October 01, 2024
  • MATOKEO YA USILI WATENDAJI WA KIJIJI.2. September 29, 2024
  • MATOKEO YA USILI WATENDAJI WA KIJIJI. September 29, 2024
  • Tazama zaidi

Habari Mpya

  • KISIMA CHA MAJI SAFI KUCHIMBWA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA YA NGORONGORO

    April 25, 2025
  • ZIARA YA MWENYEKITI WA HALMASHAURI TARAFA YA NGORONGORO.

    April 28, 2025
  • WANAFUNZI 576 WA KIDATO CHA SITA KUFANYA MTIHANI WA TAIFA NGORONGORO.

    May 06, 2025
  • MAFUNZO YA SHERIA NA UTAWALA BORA YATOLEWA KWA VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA NGORONGORO.

    March 18, 2025
  • Tazama zaidi

Video

Afisa kilimo Ngorongoro aeleza na kufafanua namna ya kupata mazao yenye afya na mbegu bora kutumia katika kilimo.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Upimaji darasa la Nne 2019
  • Taarifa na Matangazo
  • Mikataba na Miongozo
  • machapisho mbalimbali
  • Habari kwa umma
  • Taarifa kwa Umma
  • JINSI YA KUPATA SALARY SLIP
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO, VYUO VYA ELIMU YA KATI NA VYUO VYA UFUNDI JUNE 2019.
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2023 NGORONGORO

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Rais
  • Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
  • NGORONGORO DC YOUTUBE CHANEL
  • MATOKEO YA UPIMAJI DARASA LA NNE 2019 WILAYA YA NGORONGORO

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.