Chuo cha Serikali za Mitaa kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kimetoa mafunzo ya elimu ya uongozi kwa wenyeviti wa vijiji na vitongoji vyote ndani ya Tarafa ya Loliondo.
Mafunzo hayo yametolewa leo tarehe 27 Februari, 2025 kwenye ukumbi wa mkutano wa Halmashauri, hata mafunzo hayo yamefunguliwa na kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bw. Thomas Nade.
Mafunzo hayo yameangazia katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu ya utawala bora, maana ya kiongozi, muundo wa serikali za mitaa, sheria za miongozo, usimamizi wa fedha za wananchi pamoja na aina ya vikao vinavyoendeshwa katika ngazi za vijiji na vitongoji.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.