Idadi ya watoto wa kike wanaokeketwa Loliondo wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha,imepungua kufikia asilimia 75 kwa mwaka huu.
Hayo yameelezwa na Mratibu wa Afya ya Uzazi na Mtoto, Loliondo, Bi. Nailejileji Joseph katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari kwenye warsha ya wiki moja ya mafunzo juu ya Elimu ya Afya ya Uzazi na Maadili.
Warsha hiyo inajumuisha wakunga wa Jadi, Waganga wa tiba asili, viongozi wa dini, waandishi wa habari na wahamasishaji afya jamii.
Aidha wajumbe katika warsha hiyo wajumbea wamesema kuwa watoto hususani wa kike wamekuwa wakikosa haki zao za msingi ikiwemo elimu.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.