UTANGULIZI
Idara ya Maendeleo ya Jamii ni Idara mtambuka ambayo hushughulikia suala la uhamasishaji jamii na kujenga uwezo katika nyanja zote za maendeleo kupitia vitengo vyake. Pamoja na hayo, imepewa jukumu la kuratibu programu mbalimbali zinazolenga kusaidia jitihada za jamii kujilitea maendeleo ya Afya, Elimu, Maji, na Uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Aidha, Idara inafanya shughuli mbalimbali za kuhamasisha na kujenga uwezo kwa jamii kwa kuwawezesha jamii kupitia vikundi ama mtu Mmmoja mmoja kuwa na mwitikio chanya wa kufanya shughuli za maendeleo kwa kushirikishwa na idara zingine mama kama Mifugo, Kilimo, Maji, Mipango, Sheria, Ardhi na Maliasili, Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
Idara hii imegawanyika katika vitengo 4 ambazo zinawezesha Wataalamu wake kufanya kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na weledi. Pamoja na hayo, idara imepewa majukumu ya kuratibu rasmi shughuli mbalimbali zinazojitokeza kutokana na Miongozo mbalimbali ya Serikali ambayo kwayo hayapo kwenye Muundo rasmi wa Idara hii.
MUUNDO WA IDARA
-Mkuu wa Idara.
-Idara imegawanyika kwenye sehemu kama inavyooneka hapa chini.
1. Kitengo cha Mipango na Utafiti
2. Kitengo cha Jinsia na Watoto
4. Kitengo Cha Vijana
5. Kitengo cha Maendeleo ya Jamii.
Shughuli ambazo Idara inaratibu:
Uratibu wa UKIMWI
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.