Taarifa za Msingi za Idara ya Utawala na Utumishi.
Idara ya Utawala na Utumishi ni moja ya Idara zilizopewa dhamana ya kuratibu shughuli zote za utawala na maendeleo ya rasilimali watu. Kutoka mwaka 2008 hadi Mwaka 2014, Idara hii imefanikiwa kuboresha mazingira ya kazi kwa kujenga nyumba za watumishi takriban 26, na ukarabati wa ofisi 22. Ujenzi huu wa ofisi na nyumba za watumishi umelenga kuboresha mazingira ya kazi na ufanisi katika kutekeleza kajukumu.
Aidha katika kipindi hicho hicho, Idara imefanikisha kuajiri watumishi wapya 220 na kuhakikisha wanathibitishwa. Watumishi 200 wengine wamepandishwa madaraja kwa ngazi mbalimbali kwa mujibu wa taratibu za Utumishi wa Umma.
Pamoja na mafanikio hayo, zipo chngamoto za ukosefu wa wataalamu wenye sifa, hasa kwenye ngazi za chini za utawala za vijiji. Pia kata na vijiji vinapungukiwa na wataalamu wa ugani, upungufu wa nyumba za watumishi na ofisi pia.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.