Chimbuko la eneo
Halmashauri ya Wilaya Ngorongoro ni mojawapo kati ya Halmashauri za Wilaya sita na Jiji moja zilizopo katika Mkoa wa Arusha Nchini Tanzania. Makao Makuu ya Wilaya yapo Loliondo Wasso umbali wa takriban kilomita 400 kutoka Makao Makuu ya Mkoa. Wilaya hii ilianzishwa mwaka 1979 chini ya sheria namba 5 ya Mamlaka za Serikali za Mitaa ya Mwaka 1982 ikiwa na Tarafa tatu za Loliondo, Sale na Ngorongoro. Tarafa ya Ngorongoro imo kwenye eneo la Hifadhi ya Ngorongoro (NCA) iliyoanzishwa kwa Sheria Sura 413 ya mwaka1959 (NCA, CAP 284 (R.E.2002) na linasimamiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA).
Utawala na watu wake
Wilaya ya Ngorongoro inapakana na Nchi jirani ya Kenya kwa upande wa Kaskazini, Wilaya ya Serengeti kwa upande wa Magharibi, Wilaya za Monduli na Longido kwa upande wa Mashariki na Wilaya ya Karatu kwa upande wa Kusini.
Kutokana na Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012, Wilaya ya Ngorongoro ilikuwa na idadi ya watu 174,278 Wanaume wakiwa ni 82,610 na Wanawake ni 91,668 ambapo wastani wa ukubwa wa kaya ni 4.8 na ongezeko la watu katika Mkoa wa Arusha ‘growth rate’ ikiwa ni asilimia 2.9~3.
Ukubwa wa Eneo
Wilaya ya Ngorongoro ina eneo la kilometa za mraba zipatazo 14,036 ambalo lipo katika nyuzi 30030’ kusini mwa Ikweta na 35042’ Mashariki mwa Greenwich na urefu wa mita 1,009 hadi 3,645 kutoka usawa wa bahari.
Mgawanyo wa ardhi katika Wilaya ya Ngorongoro ni kama ifuatavyo:-
Hali ya hewa
Kwa ujumla Wilaya ya Ngorongoro ina maeneo ya joto la washastani hasa katika Tarafa ya Sale na hali ya Kitropikali Wilaya Ngorongoro ina mvua za wastani wa 800mm hadi 1,000mm na upepo Mkali unaovuma kutoka Mashariki kuelekea Magharibi. Maeneo makubwa ya Wilaya ya uoto wa asili jamii ya Akashia hasa ukana wa Kati, Mashariki na Magharibi. Upande wa Mashariki na Magharibi kuna Ukanda wa bonde la Ufa na misitu Mkubwa. Upande wa Kusini mwa Wilaya ni eneo maarufu la Hifadhi ya Ngorongoro linalochukua asilimia 59 ya wilaya ambalo lipo katika Tarafa moja ya Ngorongoro.
Katika wilaya hii ndipo lilipo bonde la Ngorongoro maarufu kama Ngorongoro kreta na mlima Ol-Doinyo Lengai ambapo ni aina ya milima volcano hai. Kutokana na Jiographia ya eneo na hali ya hewa sehemu ya wilaya ya Ngorongoro ndiyo kitovu cha mapitio ya nyumbu na mazalia yake hasa ikiwa sehemu ya ecolojia ya Serengeti.
Uoto wa Asili
Wilaya ina misitu minne (4) ya asili iliyosajiliwa ambayo ni:-
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.