Wilaya inalo eneo linalofaa kwa kilimo lenye kilomita za mraba 500 sawa na hekta 50,000 ambazo ni sawa na asilimia 4 ya eneo lote la Wilaya.
Katika msimu huu wa kilimo wa 2016/2017 hali ya hewa siyo ya kuridhisha kwani mvua za vuli zilinyesha chini ya kiwango yaani wastani wa mm 0.55 kwa mwezi na mvua za masika zilinyesha kwa kiwango cha chini ya wastani yaani mm 1.7 kwa mwezi wakati kwa kawaida mvua za masika huwa mm 500 au zaidi na huanza mwezi Desemba hadi April kila mwaka lakini kwa msimu huu mvua zilianza kunyesha kuanzia Januari 2017 hali inayoashiria kuwa kuna uwezekano wa kuwepo na upungufu wa chakula.
Hali hii ya ukame wa muda mrefu imeweza kusababisha pia kuwepo na upungufu wa malisho na maji kwa mifugo ila kwa sasa haliimeanza kuwa nzuri japo mifugo wengi haijawa na afya ya nzuri Utabiri wa hali ya hewa unaonesha mvua kwa kipindi cha mwezi machi zitanatarajiwa kuwa za wastani. Utabiri huu ni kwa mujibu wa Mamlaka ya hewa Tanzania.
Wilaya ina jumla ya hektari 2020 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji katika vijiji 10 Mazao yanayolimwa ni Mahindi, Ndizi, Maharage, Mbogamboga na matunda mbalimbali kati ya hektari 2020 zinazolimwa kwa sasa ni hektari 1,200. Kuanzia mwaka 2006/2007 kupitia miradi ya DADPs jumla ya mifereji 7 ya asili imekarabati ambayo imeweza kuongeza hekta 150 za umwagiliaji.
Wilaya ina Minada ya mifugo 17, ambapo kuna jumla ya minada ya awali 16 na mnada mmoja wa mpakani.Minada hii haina miundombinu inayokidhi haja, isipokuwa mnada wa Oldonyosambu na Mnada wa wasso.
Miundombinu ya majosho ni muhimu katika kudhibiti magonjwa yaenezwayo na kupe, kama; Ndigana kali, Ndigana baridi, maji kwa moyo, ambayo bado yanaendelea kusababisha hasara kwa wafugaji.
Wilaya ina majosho 31 ya kuogesha mifugo, ambapo majosho 25 ni mazima na majosho 6 ni mabovu, hivyo kuna uhitaji wa majosho 25.
Tatizo la kukosekana kwa maji katika baadhi ya maeneo, imechangia zoezi la kuogesha mifugo kutofanikiwa kwa asilimia kubwa, hivyo kupelekea wafugaji wengi kutumia bomba za mikono katika zoezi la uogeshaji wa mifugo.
Wilaya ina malambo ya mifugo 20, ambayo yote ni ya msimu wa masika na kwa kipindi hiki cha kiangazi karibu malambo yote hukauka. Vilevile malambo mengine yanahitaji marekebisho ya mara kwa mara ya kupunguza udongo unaotuwama ndani yake. Katika kipindi cha kiangazi wafugaji hutegemea maji kutoka kwenye mito na visima vya kuchimba.
Uboreshaji wa mifugo umekuwa ukifanyika kwa kununua madume kutoka taasisi za serikali na mashamba mbalimali ya mifugo mfano Manyara ranch, West Kilimanjaro na Mpwapwa. Misaada mingi ni kupitia wadau mbalimbali wa maendelea ndani ya Wilaya.
Kwa mwaka 2015/16 madume 71 ya ng’ombe yamenunuliwa na kugawiwa kwa jamii husika. Madume haya yamenunuliwa na NCAA Madume 40, Shirika la PWC Madume 12, Shirika la Palisep/Oxfam madume 8 na Mradi wa DADPs Madume 11.
Hata hivyo Shirika la Palisep/Oxfam wameweza kununua Mitamba ya Ng’ombe 117 kutoka nchini jirani ya Kenya, kwa wananchi wa kata ya Enguserosambu ikiwa na lengo la kuongeza upatikanaji wa lishe bora kwa maana ya maziwa kwa familia zisizo na uwezo.
Halikadhalika wafugaji wameendelea kuboresha mifugo yao kwa kununua madume ya mbegu aina ya Sahiwal kwa ng’ombe, madume aina ya Galla kwa mbuzi na Madume aina ya Doppers kwa kondoo kutoka mashamba ya mifugo nchini Kenya.
Hali ya afya ya mifugo sio ya kuridhisha kwa sasa kutokana na kumalizika kwa kipindi cha ukame. Kutokana na mvua zinazoendelea kwa sasa afya inategemewa kuimarika kadri malisho na maji yanavyozidi kupatikana.
Magonjwa ya mifugo yameendelea kuwa tishio sana kwa wilaya ya Ngorongoro hasa ugonjwa wa mapafu kwa ng’ombe, ugonjwa wa miguu na midomo kwa ng’ombe, ugonjwa wa kutupa mimba, Ugonjwa wa vipele kwa ng’ombe, ugonjwa wa kimeta , ugonjwa wa mapafu kwa mbuzi na ugonjwa wa sotoka kwa mbuzi/kondoo.
Magonjwa haya yameendelea kuwa tishio kutokana na serikali kutoagiza chanjo kutoka nchi ya Ethiopia/Botswana, kama ilivyokuwa miaka ya nyuma na kupelekea wafugaji kutumia chanjo kutoka Kenya ambazo simeonekana kutokuwa na ubora.
Ili kuweza kutatua changamoto za magonjwa Halmashauri imeanzisha mfuko unaojiendesha (Revolving Fund), ili kuakikisha huduma ya chanjo inapatikana karibu na wananchi. Mfuko huu utagharimia ununuzi wa chanjo za magonjwa mbalimbali ya mifugo.
Kwa kuanzia Halmashauri imetenga jumla ya shilling 10,000,000, za kuingiza chanjo kutoka Botswana kwa kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.