HUDUMA YA MAJI MJINI
Huduma ya usambazaji maji mjini ipo chini ya Mamlaka ya Maji ya Mji Mdogo wa Loliondo (Loliondo Urban Water Supply and Sanitation Authority – LOLIONDO UWSA). Kata mbili za Orgosorok na Oloirien na vijiji vitatu vya Loliondo, Sakala na Wasso vinahudumiwa.
Huduma ya maji imewafikia wakazi 9,710 kati ya wakazi 15,140 sawa na asilimia sitini na nne (64%). Kuna zaidi ya maunganisho 400 ya majumbani, sehemu za Taasisi na sehemu za biashara, na kuna jumla ya vituo vya umma vya maji kumi na moja (11).
HUDUMA YA MAJI VIJIJINI
Huduma ya maji vijijini imewafikia wakazi 97,132 kati ya wakazi 174,278 wa vijijini sawa na asilimia 56. Wilaya ina jumla ya miradi 146 ya maji ambapo kuna miradi 32 ya mtiririko, 6 ya kusukumwa kwa pampu, visima virefu 64 na matanki 45 ya maji ya mvua
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.