Idara ya Elimu Msingi ni moja ya Idara 13 zinazotekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Idara hii imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutoa huduma ya elimu ya Msingi kwa watoto. Kwa mwaka wa fedha 2016/2017 Idara inaratibu shule za Msingi 67 ambapo , shule 62 zinamilikiwa na serikali na shule 5 zinamilikiwa na sekta binafsi. Kuna jumla ya wanafunzi 29,121 ambapo 16,246 ni watoto wa kiume na 12,875 ni watoto wa kike. Pamoja na changamoto za upungufu wa miundombinu n walimu , hali ya ufaulu imezidi kupanda ambapo kwa mwaka 2014 na 2015 asilimia ya ufaulu ni 73.5
Suala la kujiunga na elimu ya msingi ni asilimia 97% na haya ni mafanikio makubwa ambapo asilimia ya mdondoko wa wanafunzi ni 7 tu. Hii inaleta changamoto kwa wananchi kwamba miaka ya karibuni Halmashauri itaondokana na jamii isiyouwa na maarifa ambayo kwa mwaka 2017 ipo asilimia 52.5.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.