Fursa za uwekezaji katika Utalii ikiwa ni kuwekeza katika Hoteli na Kambi za kitalii.
Fursa iliyopo: Ujenzi wa Hoteli mbili and kambi za Kitalii sita katika maeneo ya Arash na Engaresero.
Maeneo yanayotarajiwa: Uwepo wa eneo la takribani hecta 76 katika vijiji viwili zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa hoteli na kambi za kitalii. Maeneo hayo yana maji ya kutosha na ni vivutio kwa shughuli za kitalii kama vile mlima Oldonyo Lengai ambao ni mlima volcano hai. Maporomoko ya maji mto Pinyinyi, chemchem ya maji moto katika maeneo ya ziwa Natron ambalo ni Pori tengefu.
Hali ya soko: Mapito ya watalii kuelekea maeneo ya mbuga ya Taifa Serengeti na Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro.
Walengwa: utalii wa ndani na utalii wa nje.
Mapendekezo kwa wawekezaji: wawekezaji wote wa ndani na nje wanaweza kuwekeza katika hii hili kutoa huduma za kitalii na kwa jamii.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.