https://youtu.be/1CNn2gx2Ayw?si=eXDCG9OUlfxsdir-
Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Brigedia Jenerali amefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali wilayani hapa, na kutoa rai kwa Wananchi kuhakikisha wanasimama kidete kuilinda na kusimamia miradi hiyo kwa ajili ya watoto wao wa sasa na vizazi vijavyo.
Akizungumza wakati ziara hiyo Brigedia Jenerali Sakulo akiwa katika shule ya msingi Samunge alipotembelea kukagua ujenzi wa madarasa mawili yenye thamani ya shilingi milioni 50 amesema Serikali imekua ikitoa fedha za kutosha kujenga na kuboresha miundo mbinu ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi wake hivyo wazazi wawapeleke watoto shule kwa wingi kwani changamoto ya madarasa haipo tena.
Aidha, katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ameambatana na wataalamu kutoka Halmashauri, Mkurugenzi Mtendaji na kamati ya usalama ketembelea chuo Cha Veta Ngorongoro, mbwalo la wanafunzi shule ya Sekondari Samunge, shule mpya ya Maalon Sekondari ambayo Serikali ilitoa kiasi cha shilingi milioni 584.2 kukamilisha ujenzi wa shule hiyo pamoja na mradi wa ujenzi tenki la maji la Mageri litakalo hudumia vijiji nane.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.