Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Bw. Murtallah S. Mbillu amesema kuwa jumla ya wanafunzi 3,521 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza kwa mwaka 2026 katika shule za sekondari wilayani humo, Kati ya wanafunzi hao wavulana ni 1,974 na wasichana 1,547.
Amesema hayo akiwa ofisini kwake leo tarehe 9 Januari 2026, pia ameongeza kwa kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan tayari ametoa fedha kwa ajili ya chakula cha wanafunzi wa shule za bweni. Huku akiweka wazi kuwa shule zote za sekondari za bweni na uongozi wa shule zote umejiandaa vyema kuwapokea wanafunzi wote waliochaguliwa.
Aidha, Bw. Mbillu ametoa wito kwa wazazi na walezi wenye watoto waliofaulu kujiunga na Kidato cha Kwanza kuhakikisha wanawapeleka shuleni kabla ya tarehe 13 Januari 2026, siku ambayo shule zitafunguliwa rasmi ili wanafunzi waanze masomo yao kwa wakati.
Akiweka msisitizo katika Suala la elimu amewataka Maafisa Elimu wa Kata kusimamia kwa ukaribu na ufanisi mkubwa la kuhakikisha wanafunzi wote wanafika na kuwasili katika shule walizopangiwa kabla ya siku za masoma kuanza.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.