Baraza la mkutano wa bajeti limepitisha na kupongeza bajeti iliyopendekezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kwa kuzingatia nyanja zote za utekelezelaji wa shughuli za Serikali.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro Mhe. Mohamed Bayo amewataka wataalam wa makusanyo ya mapato kuongeza bidii katika makusanyo ya mapato na kuziba mianya yote ya upotevu na kutobweteka kwa ongezeko la makusanyo .
Mhe. Bayo amesema hayo wakati akifungua mkutano wa baraza la bajeti la halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro ambao ni mahsusi kwaajili ya kujadili na kupitisha rasimu ya bajeti ya mwaka wa fedha ujao wa 2025/26 uliofantika leo tarehe 14/2/2025 ukihusisha waheshimiwa madiwani, wataalam kutoka vitengo na Divisheni na Vitengo mbalimbali vya halmashauri, viongozi wa taasisi mbalimbali ikiwemo TRA, TANESCO, TARURA NA RUWASA pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya.
Halmashauri imefanikiwa kusanya zaidi ya Shilingi billioni 2.226 sawa na 62.1% ya makadirio ya mapato na matumizi hadi kufikia mwezi Desemba 2024 kutoka vyanzo vya ndani ikiwa ni robo ya pili tu ya mwaka wa fedha 2024/25 ikiwa imefanya vizuri zaidi ikilinganishwa na kipindi kama hiki cha mwaka wa fedha 2023/24 ambapo halmashauri ilikua imekusanya kwa asilimia 46.4
Aidha Kwa upande wake Bi. Emmy Hongoli ambae ni Afisa Mipango Wilaya wakati akiwasilisha rasimu ya mapendekezo ya mapato na matumizi kwa maana ya bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026 kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji amesema halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro inakisia kukusanya na kupokea kiasi cha Tsh.41,280,018,526 .
Pia, halmashauri kwa mwaka huo fedha imejipanga katika vipaumbele kuu saba ambavyo ni utawala bora, kuboresha huduma za elimu, huduma za afya, kuongeza mapato ya ndani kwa kuimarisha na kusimamia mifumo ya ukusanyaji mapato, kuimarisha huduma za mifugo na kilimo, kuimarisha shughuli za uhifadhi na utalii na kuwezesha jamii kiuchumi ikiwemo kutoa mikopo isiyo na riba kwa makundi mbalimbali
Bi. Emmy Hongoli ameeleza rasimu ya bajeti hii imeandaliwa kwa kuzingatia miongozo mbalimbali ambayo ni muongozo wa bajeti wa mwaka 2025/26, ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi 2025, na mpango mkakati wa halmashauri wa miaka mitano 2021/26, mpango wa Taifa wa maendeleo wa miaka mitano, malengo ya maendeleo endelevu ya mwaka 2020-30 mambo mtambuka na maelekezo mengine ambapo Baraza limepokea kujadili kupongeza na kuipitisha.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.