Zimesalia siku nane pekee kabla ya kufanyika kwa zoezi muhimu la uchaguzi mkuu nchini. Wananchi wote wanakumbushwa kuwa tarehe 29 Oktoba 2025 ni siku maalumu ya kutekeleza haki yao ya kikatiba kwa kushiriki katika kupiga kura.
Ni wajibu wa kila mwananchi mwenye sifa na aliyejiandikisha kuhakikisha anatoka na kadi yake ya mpiga kura siku hiyo. Kadi hiyo ni ushahidi muhimu unaokuruhusu kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kuchagua viongozi wanaofaa kuliongoza taifa na jamii yako.
Ushiriki wa wananchi katika uchaguzi ni nguzo kuu ya demokrasia. Kila kura ina thamani kubwa, kwani ndiyo sauti ya wananchi katika kuamua mustakabali wa maendeleo na uongozi bora wa nchi. Kutokupiga kura ni kuacha wengine wafanye maamuzi kwa niaba yako.
Kwa hiyo, Wananchi wote kwa wingi wenu jitokezeni siku ya uchaguzi, nenda kituoni ukiwa na kadi yako ya mpiga kura na utimize wajibu wako wa kikatiba. Kumbuka, “Kura yako ni haki yako, Jitokeze kupiga kura.”
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.