Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Mohammed Bayo kwa niaba ya Waheshimiwa madiwani amesema Serikali ya awamu ya sita imefanya mambo makubwa kwa kutekeleza miradi ya maendeleo katika tarafa za Loliondo, Sale na Ngorongoro.
Mhe. Bayo ameyasema hayo wakati wa mkutano wa Baraza la Halmashauri huku Waheshimiwa madiwani wakiunga mkono na kumpongesa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanya mambo makubwa kwa kipindi cha miaka nne.
"Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliipatia Halmashauri fedha nyingi za miradi mbalimbali ya maendeleo, mpaka sasa tumefanikiwa kuwa na Zahanati 27, Vituo vya Afya sita na Hospitali ya Wilaya moja, huku Divisheni ya Elimu msingi tumepata shule mpya nne, ambapo imepelekea kufikisha idadi ya vyumba vya Madarasa 669, huku Shule za Sekondari wilayanu hapa ni 19" amesema Mhe. Bayo.
Aidha, Mwenyekiti wa Halmashauri amesema kuwa kwa muda miaka minne ya Mheshiwa Rais Samia ametoa fedha za ujenzi wa mabweni 77, matundu ya vyoo 339 huku meza na viti mpya nj 11,456.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.