Baraza la mji mdogo wa Loliondo likiongozwa na Mathey S. Kereto ambaye ni mwenyekiti wa Baraza hilo kwa kipindi cha robo ya pili limejadili na kuweka mikakati ya kuongeza mapato na kuweka mipango yenye tija ndani ya mji mdogo katika nyanja tofauti ikiwemo kubiresha hali ya kilimo, hali ya afy kwa wananchi, hali usafiri wa mazingira katika makazi na barabara pamoja na utunzaji wa mazingira kwa kuweka sheria zitakazolinda uharibifu unaosababishwa na shughuli za kibinadamu pamoja na kuongeza vyanzo vya mapato na kusimamia vyema vyanzo vilivyopo ili kulinda mapato yanayopotea.
Baraza hilo limefanyika leo tarehe 19 Februari, 2025 katika ukumbi mdogo wa halmashauri kilichojumuisha wajumbe, wataalamu wa halmashauri pamoja na Mtendaji wa mamlaka ya Mji mdogo wa Loliondo Bw. Charles Maliki.
Aidha, wajumbe wametoa wito kwa wataalamu kuendelea kufanya kazi kwa weledi na uaminifu ili kucjochea kasi ya maendeleo ya mji mdogo na halmashauri kwa ujumla pia wamewataka viongozi kuwa mstari wa mbele kusimamia malighafi na maslahi yote ndani ya mji mdogo.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.