Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mhe.Raymond Mwangwala ameendelea ziara ya Siku ya pili ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo na kusikiliza na kutatua kero za wananchi ndani ya Kata ya Sale
Akikagua Zahanati ya Sale Mhe.Mwangwala amesema serikali imeendelea kuboresha Huduma ya Afya kwa wananchi na Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan alitoa kiasi cha Millioni 500 kwaajili ya kumalizia maboma ya Zahanati ya Sale yaliyoanzishwa Kujengwa kwa nguvu za wananchi na sasa vimeletewa vifaa vya Maabara na Upasuaji vyenye thamani ya Million 84.
"Baada ya Wiki mbili nataka kuona Huduma ya Upasuaji na maabara inaanza kufanya katika kituo hiki,Wananchi waanze kupata Huduma kwa Karibu na Haraka" alisema Mwangwala
Naye Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Sale Bi.Yasinta Ngondo amemeleza kuwa wamewapokea wataalamu walioajiriwa na Serikali mwaka huu 2023 ambao ni mtaalamu mabara mmoja na wauguzi saba ambao wameshawasili na kuanza kazi
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.