Ikiiwa ni jitihada za kuboresha elimu katika Wilaya ya Ngorongoro Idara ya elimu Wilaya ya Ngorongoro imekaa kikao leo tarehe 01 Februari 2024 kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Maria Correson
kikao hicho kimehusisha Maafisa elimu Kata, Wakuu wa Shule za Sekondari pamoja na Wakuu wa Shule za Msingi. Huku wazungumzaji wakuu wakiwa ni Afisa Elimu Msingi Wilaya ya Ngorongo Bi. Mwanamina Muro pamoja na Afisa Elimu Sekondari Bw. Emmanuel Sukumus akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro
Kikao hicho kimelenga kupeana mrejesho wa majukumu yaliyofanywa,kuweka mikakati pia kukumbushana majukmu ya kielimu ndani ya Wilaya. Afisa elimu shule za sekondari Wilaya ya Ngorongoro Bw.Emmanuel Sukumus amewaasa walimu kusimama na kutekeleza Majukumu kama viongozi katika kutatua changamoto mbalimbali zinazo wakabili wanafunzi Kwa kuzingatia utawala wa Sheria
"Kwasababu nyie ni viongozi mnafursa nyingi sana za kusimamia changamoto zilizopo chini yenu ikiwa ni pamoja na wanafunzi mnaowapatia elimu hivyo chochote mtakachokifanya kizingatie Utawala na Sheria, kuna miongozo mbalimbali, kuna Sheria mbalimbali pia kuna taratibu mbalimbali tafadhali simamia na kufuata miongozo mbalimbali iliyowekwa na Utawala wako" amesema Sukumus
Aidha Afisa elimu Msingi Wilaya Bi. Mwanamina Muro amewapongeza walimu Kwa jitihada zao Kwa ongezeko la kitaaluma katika kufaulisha wanafunzi na kuwakumbusha kuongeza juhudi zaidi katika kukabiliana na chamoto ili kufikia malengo ya Mkoa ikiwa ni wastani wa asilimia 95. Hivyo Bi. Muro ameainisha mjongeo wa ufaulu Kwa darasa la nne na darasa la Saba Kwa mwaka 2021, 2022 na 2023.
"Darasa la Saba Kwa Mwaka 2022 tulifaulisha Kwa asilimia 68.25, Mwaka 2022 tukaongeza Kwa asilimia 69.71 ambapo tulikuwa na mjongeo wa asilimia 1.46 lakini mwaka 2023 tulipata mjongeo wa asilimia 8.2 na Kwa darasa la nne mwaka 2021 tulikuwa na asilimia 72.4 , mwaka 2022 tulipanda Kwa asilimia 73.37 lakini Kwa mwaka 2023 tumeongeza ufaulu Kwa asilimia 7.4 ni Imani yangu kwamba mwaka huu tutaenda kufanya vizuri zaidi pia mkiwa kama viongozi msikwamishwe na changamoto bali mtatue changamoto" amesema Bi. Muro
Ikumbukwe shule kumi bora zilizoongoza Wilaya ya Ngorongoro ni Butemine, Loresho, Endulen, Nainokanoka, Lumo, Bright, Maria Correnson, Loliondo G.C.C.T, Digodigo G.C.C.T na St.Luke.
Hata hivyo Bi. Muro amewasihi walimu kuongeza jitihada za kitaaluma Kwa kuhakikisha wanafaulisha Kwa madaraja yote, ili kuweza kuachana na ufaulu wa daraja C pekee na kwenda kwenye ufaulu wa daraja B na daraja A.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.