Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Mohammed Bayo na Mkurugenzi mtendaji Bw. Murtallah S. Mbillu leo tarehe 25 Aprili, 2025 kwa pamoja wamefanya ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo tarafa ya Ngorongoro, huku shule ya sekondari ya wasichana Ngorongoro ikiwa ni moja eneo lilofikiwa na ziara hiyo.
Mkurugenzi ametoa ahadi mbele ya wanafunzi hao kuwa muda si mrefu maji ya uhakika yatapatikana shuleni hapo kwani taratibu zote zilishafanyika kilichobaki ni kisima cha maji safi kuchimbwa.
Aidha, Mwenyekiti wa Halmashauri ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa uongozi wa Halmashauri, Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro wanaendelea na jitihada za kumaliza changamoto zote shuleni hapo, huku Mh. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameshatoa maelekezo miundombinu yote katika shule hiyo iendelezwe ikiwemo umaloziaji wa mabweni ya wanafunzi
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.