Mwenyekiti wa Halmashauri Wilaya ya Ngorongoro Mhe. Mohamed Bayo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hasani kwa kufuta tangazo lililokuwa linazuia Wananchi wa tarafa ya ngorongoro kushiriki katika zoezi la uchaguzi wa Serikali za mitaa.
Amebainisha hayo leo ijumaa tarehe 18 oktoba 2024 wakati akifungua mkutano wa Baraza la Halmashauri kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/2025 yani mbapo amewahakikishia wakazi wa wilaya ya Ngorongoro kwa ujumla kua Halmashauri imeweka mikakati ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa kubadilisha matumizi baadhi ya fedha kutoka katika miradi mingine ili kuleta maendeleo katika tarafa zote wilani hapa Baraza limeazimia kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta za afya, elimu, miundombinu ya barabara na maji.
Aidha, katika kipindi cha Julai hadi Septemba Mhe. Bayo amesema Halmashauri imekusanya mapato kwa asilimia 32 ya makadirio ya kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 3.58 kwa mwaka wa fedha 2024/25 kutoka katika vyanzo mbalimbali huku akiwataka wataalamu wa Halmashauri kutobweteka na mafanikio hayo ya makusanyo wafanye kazi kwa bidii ili kufikia lengo la makusanyo la mwaka ili kutekeleza kwa ukamilifu miradi ya maendeleo, kuinua wananchi kiuchumi pamoja na utekelezaji wa afua mbalimbali ikiwemo afua za lishe.
Pia katika hotuba yake amesema kuwa zoezi linaloendelea la uandikishaji wapiga kura katika orodha mpiga kura zaidi ya asilimia 95 ya Wakazi wamejiandikisha.
Ametumia fursa hiyo kuwasihi madiwani kuhimiza wananchi katika kata zao kujiandikisha kwa wingi ili wasikose haki yao ya kupiga kura na kuwachagua viongozi wa kuwaletea maendeleo katika vijiji, vitongoji na mitaa yao.
Katika hatua nyingine Baraza limetambua mchango unaotolewa na wahisani wa maendeleo (KFW) kuendelea kuleta miradi ya maendeleo na kuongeza kasi kwa miradi wanayoendelea kuitekeleza wilayani Ngorongoro na kuikamilisha kwa wakati ili zianze kutumiwa na Wananchi.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.