Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya Bw. Thomas Nade ameongoza zoezi la ugawaji wa mitungi ya gesi kwa kundi la wajasiriamali la akina mama lishe na akina baba lishe kama kampeni ya kuhamasisha matumizi bora ya nishati safi wilayani Ngorongoro.
Bw. Nade amewaomba wajasiriamali hao kwenda kuwa mabalozi wazuri wa kuhamasisha wengine kupendelea kutumia nishati gesi kwenye matumizi ya kupikia na kuachana kabisa na matumizi ya mkaa na kuni ili kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye amekua mstari wa mbele katika kuwahimiza Watanzania kujikita katika matumizi ya nishati safi.
Aidha, mkakati wa nishati safi unalenga kutoa mwongozo wa namna ya kupunguza athari za kiafya zinazisababishwa na nishati chafu, inapunguza muda wa matumizi kwa mtumiaji pia husaidia kulinda mazingira na kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.