Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mhe. Raymond Mwangwala ameipongeza kampuni ya utalii ya TAASA kwa ujenzi wa bweni la wavulana katika shule ya msingi Ololosokwan" Ujenzi bweni hili jipya umesadia kupunguza mrundikano wa wanafunzi bwenini katika shule hii ya Msingi Ololosokwan" amesema Mhe.Mwangwala
Mhe. Mwangala amesema hayo wakati wa taasisi inayojushughulisha na utalii ya TAASA ikikabidhi bweni kwa shule ya Msingi Ololosokwan ikiwa ni matokeo ya juhudi ya serikali ya awamu ta sita kuimarisha sekta yautalii ambapo wadau wa sekta hiyo wamenufaika na kushiriki katika gurudumu la maendeleo
"Tunamshukuru Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan, sasa tunaona matokeo ya TANZANIA THE ROYAL TOUR kwani leo hii tunakabidhiwa Bweni la wavulana lenye thamani ya Milioni 89 zilizotolewa na watalii waliotembelea shule hii" amesema Mhe Mwangala
Vilevile Mhe.Mwangwala amesema Serikali inampango wa Kuifanya shule hiyo kuwa ya Bweni kwa wanafunzi wote ili kuwapa fursa wanafunzi wote waweze kuhuduria masomo yao vyema ambapo amewataka viongozi hasa watendaji wa vijiji, kata na Maafisa Elimu kata kuahikikisha wanasimamia watoto waliofikia umri wa Kwenda Shule wanaandikishwa na waliofaulu kujiunga na Kidato cha kwanza 2023 wawe wameshajiunga na kidato cha kwanza katika shule za Sekondari
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.