Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Missaile Albano Musa ameipongeza halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kwa kuhahakikisha wanakusanya vema mapato ikiwemo matumizi sahihi ya bakaa katika miradi mbalimbali ya maendeleo na kusisitiza mikopo ya asilimia kumi ya fedha hizo zitengwe ili kuwezesha wanawake, vijana na makundi maalum kupata mikopo
Musa ametoa pongezi hizo wakati wa kikao maalum cha Baraza la Madiwani wilaya ya Ngorongoro cha kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2024/2025 ambapo halmashauri hiyo imepata hati safi.
"Kusanyeni fedha na miradi ya maendeleo itekelezeke, nawapongeza kwa kupata hati safi na kuendelea kupunguza hoja mpaka kufikia hoja tisa (zikiwemo zile za kisera) lakini ni lazima kuzitafutia majibu ili zifutwe." Amesema Katibu Tawala huyo.
Naye Mkurugenzi wa halmashauri ya Ngorongoro, Murtalla Mbilu amesema kuwa siri ya mafanikio hayo ni usimamizi mzuri na kutekeleza maelekezo na maagizo ya uongozi wa Mkoa pamoja Mkaguzi na Mdhibiti wa hesabu za Serikali pamoja na kuzuia ubadhirifu, ufisadi na uzembe kwa watumishi na kuongeza ushirikiano.
Amesema halmashauri hiyo imekusanya zaidi ya shilingi bilioni 3 ambayo ni zaidi ya asilimia 100 katika sekta mbalimbali kwaajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa mwaka huu wa fedha
Aidha, Mkaguzi Mkuu wa Nje Mkoa Mkoa wa Arusha, Valence Rutakyamirwa licha ya kuipongeza halmashauri hiyo kwa kuweka uwiano mzuri na majibu ya hoja kwa ufanisi ikiwemo kupata hati safi ya ukaguzi, ameitaka halmashauri hiyo kuhakikisha madeni ya wakandarasi waliotoa huduma ya vyakula shuleni na wazabuni yanalipwa kwa wakati.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.