Imeelezwa kuwa, Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ambaye kwa sasa ni mgombea wa Urais kupitia CCM, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan ameidhinisha mpango wa ujenzi wa barabara ya kutoka Kigongoni Mto wa Mbu mpaka Loliondo wilaya ya Ngorongoro,yenye urefu wa Km 217.
Hayo yamethibitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla, mara baada ya kupokea ombi kutoka kwa wananchi wa Ngorongoro, kwenye Mkutano wa hadhara, uliofanyika Kata ya Sale Jumanne ya leo, Septemba 02, 2025.
CPA Makalla amesema kuwa, ujenzi wa barabara hiyo unatekelezwa kwa awamu nne, ambapo awamu ya kwanza tayari imeshakamilika kwa kujengwa barabara ya kiwango cha lami yenye urefu Km 49 kutoka Sale mpaka Waso kwa gharama ya shilingi bilioni 87.
Utekelezaji wa awamu ya pili tayari ujenzi wa bararabara ya Km 10 kutoka Waso kwenda Loliondo, mradi ambao umeanza kutekelezwa kwa gharama ya shilingi bilioni 12.
Awamu ya tatu ni barabara ya Mto wa Mbu - Engaruka Km 50 ambapo imegawanyika Mto wa Mbu - Selela Km 23 taratibu za kumapata Mkandarasi zinakamilika aanze ujenzi, awamu hiu ni Selela - Engaruka yenye urefu wa Km 27, usanifu umekamilika na Serikali iko tayari kupata Mkandarasi kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi huku awamu ya mwishi ni Engaruka mpaka Ngaresero Km 24 nayo usanifu umekamilika Serikali imetangaza zabuni ili kumpaka mkandarasi.
"Nataka niweke wazi, barabara yote ya Km 217, Serikali ya CCM inayo nia ya dhati, kuhakikisha changamoto hiyo inatatuliwa na kuondosha kero kwa wakazi wa Ngorongoro, nimekutana na Meneja wa TARURA Mkoa, ninaahidi nitasukuma jambo hili ili ahadi ya chama cha Mapinduzi iweze kutekelezwa"Amesisitiza CPA Makalla.
Awali, wananchi wabainisha kuwa kakamilika kwa ujenzi babarabara hiyo ambayo inaunganisha wakazi wa Wilaya ya Monduli na Ngorongoro, licha ya kurahisisha usafiri zaidi itakuwa chachu ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wakazi wa wilaya hizo, ambazo asilimia kubwa ni wakulima na wafugaji.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.