Daraja la Mto Mmbaga limekamilika kujengwa katika Kata ya Oldonyosambu kwa lengo la kurahisisha usafiri kati ya Kata za Sale, Pinyinyi na Oldonyosambu. Daraja hilo pia limekuwa kiunganishi muhimu kati ya Kijiji cha Jema na Kijiji cha Oldonyosambu, ambako awali wananchi walikuwa wakikosa mawasiliano hasa nyakati za mvua kutokana na maji ya mto huo kujaa na kusababisha eneo hilo kushindwa kupitika.
Ujenzi wa daraja hilo ulianza tarehe 23 Februari 2025 kwa ufadhili wa Serikali, ambapo kiasi cha shilingi milioni 500 kilitolewa kugharamia mradi huo hadi kukamilika kwake. Hatua hii imekuwa suluhisho la kudumu kwa changamoto za usafiri na mawasiliano zilizokuwa zikiwakabili wakazi wa maeneo hayo kwa muda mrefu.
Kati ya fedha hizo, shilingi milioni 268.2 zilitumika kujenga daraja la upinde wa mawe, huku shilingi milioni 231.7 zikielekezwa katika ujenzi wa barabara ya kiwango cha moramu yenye urefu wa kilomita 5.2, upanuzi wa barabara, pamoja na ujenzi wa makaravati matano ya zege na karavati moja la mawe. Miundombinu hiyo inatajwa kuongeza urahisi wa usafirishaji wa watu na bidhaa katika vijiji hivyo.
Wananchi wa vijiji vya Jema na Oldonyosambu wametoa shukrani zao kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jitihada za kuboresha miundombinu ya barabara, huku wakieleza kuwa kukamilika kwa daraja hilo kutachochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa kurahisisha huduma za kijamii na shughuli za kibiashara katika maeneo hayo.
@rc_mkoa_arusha @halmashauri_ya_karatu @muleba_dc @merudistrictcouncil2 @dc_ngorongoro @longido_district_council @arusha_district_council @maelezonews
https://www.instagram.com/p/DO-8nAvDHEv/?igsh=OGl0ZnUzczl1bw==
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.