Tunapenda kuwatangazia wananchi wote kuwa ,kutakuwepo na zoezi la Kitaifa la ugawaji wa dawa za KingaTiba,dhidi ya ugonjwa wa macho wa Trakoma (Vikope) awamu ya nne. kwa watu wote kuanzia watoto wenye umri wa miezi sita mpaka wazee, kuanzia tarehe 10.10.2018 hadi 14.10.2018
Dawa hizi zitatolewa na wagawa dawa waliopewa mafunzo maalumu kutoka kila Kitongoji ,ambao watapita nyumba kwa nyumba na katika maboma kumezesha dawa.
Dawa hizi za KingaTiba zitatolewa bure kwa wananchi.
Tunaomba watu wote kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi hili ili kwa pamoja tuweze kutokomeza ugonjwa huu unaosababisha upofu.
‘USICHUKULIE POA, TRAKOMA INAZUILIKA, MEZA KINGATIBA’
Afya bora kwa maendeleo ya jamii na Taifa
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.