Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Bw. Murtallah S. Mbillu, amewaongoza watumishi wa Halmashauri hiyo katika zoezi la kufanya usafi na kutunza mazingira katika Hospitali ya Wilaya ya Ngorongoro. Zoezi hilo limefanyika leo, Jumatano, tarehe 13 Agosti 2025.
Shughuli hiyo ilihusisha usafi wa maeneo ya nje ya majengo pamoja na mazingira ya ndani ya hospitali, ikiwa na lengo la kuboresha hali ya usafi na afya ya sehemu ya kazi. Watumishi wameshiriki kikamilifu kuhakikisha maeneo yote yanakuwa safi na salama kwa wagonjwa na wageni wote wanaofika hospitali.
Zoezi hilo limehusisha Wakuu wa Divisheni, Wakuu wa vitengo mbalimbali pamoja na watumishi wengine wa Halmashauri. Ushirikiano huo umeonekana kuwa mfano mzuri wa mshikamano na uwajibikaji katika utunzaji wa mazingira ya taasisi za umma.
Akizungumza wakati wa shughuli hiyo, Bw. Mbillu ametoa shukrani za dhati kwa watumishi wote waliojitokeza na kushiriki kuanzia mwanzo mwa zoezi la usafi mpaka kumalizika.
https://www.instagram.com/p/DNTKseXskWe/?igsh=Mm01ZzJvNXRqdHI=
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.