Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Kata jimbo la Ngorongoro, Mkoa Arusha wametakiwa kufuata, kanuni na miongozo ya Tume huru ya uchaguzi ili kuufanya uchaguzi wa mwaka huu kuwa huru na wahaki.
Hayo yamesemwa leo na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ngorongoro, Bw Emanule Laban Mchome wakati akifungua semina ya siku tatu ya mafunzo kwa maafisa wasaidizi ngazi ya Kata kwa jimbo la Ngorongoro yanayoendelea kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Ngorongoro
“Nawaasa wana mafunzo wote kuhakikisha kuwa kanuni, taratibu na miongozo ya ya Tume huru ya uchaguzi inafuatwa ili kuondoa malalamiko kwa wadau wa uchaguzi na vyama vya siasa” amesema Mchome
Amesema kuwa anaimani kubwa na maafisa wote ambao watashiriki kwenye zoezi hili kubwa la kupata viongozi kwa upande wa Rais, Ubunge na Udiwani.
Mafunzo haya ya siku tatu yanaendeshwa na maafisa wasaidizi ngazi ya Jimbo la Ngorongoro kwa malengo ya kuongeza uelewa kuhusu uchaguzi na kujifunza mambo Mahsusi yanayotakiwa kuyafuata.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.