Afisa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Bi. Tumaini Saoyo akizungumza na Watumishi wa makao makuu wakati wa kikao kilichohitishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bw. Murtallah S. Mbillu.
katika kikao hicho Bi. Tumaini ametumia nafasi hiyo kuwahimiza na kuwataka Watumishi hao kujitokeza kwa wingi siku ya kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura kwa ajili ya kushiriki katika zoezi la uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili waweze kuchagua viongozi sahihi watakaoleta maendeleo yenye tija kwa jamii.
Aidha, Bi. Tumaini ametumia nafasi hiyo kutoa elimu kuhusu sifa za mpiga kura na mgombea Pamoja kutoa ufafanuzi wenye utofauti kati ya zoezi la uboreshaji na kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura na kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura kwa ajili ya kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
“uboreshaji wa taarifa za kitambulisho cha mpiga kura na kuandikisha wapiga kura wapya kwenye daftari la kudumu ni zoezi linalosimamiwa na Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwakani 2025 na zoezi hili liatakaloanza mwezi wa kumi mwaka huu ni maalumu kwa ajili uandikishaji wa wananchi kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa”
Ikumbukwe zoezi la uandikishaji Wilaya ya Ngorongoro litaanza mnamo tarehe 11 hadi tarehe 20 Oktoba 2024.
“Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze Kushiriki Uchaguzi”
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.