BARABARA YA WASSO-LOLIONDO KM 10 KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI KUANZIA MWEZI DECEMBER MWAKA HUU
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongela leo katika kikao cha Maendeleo ya Mkoa (RCC) kilifanyika jijini Arusha
Mongela amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu hasani amekwisha kutoa fedha kwaajili ya barabara hiyo kutengenezwa ambapo amesema kinachosubiriwa ni utaratibu wa kumpata mkandarasi, hata hivyo Mongela amesema hadi kufikia mwezi wa Desemba mwaka huu wa 2022 barabara hiyo itakuwa imekwishanza kwa kuwa michakato yote ipo katika hatua za mwisho
Akizungumza na mwandishi wetu, mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ngorongoro Mhe. Mohammed Bayo Marekani ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Ologosorock ambapo inachukua eneo lote la kilomita 10 zitakazotengenezwa kwa kiwango cha Lami, amemshukuru Mhe. Rais kwa maamuzi hayo ya kutengeneza barabara hiyo ambapo amesema kutengenezwa kwa Barabara hiyo kutaufanya mji wa Loliondo ambao ndio makao makuu wa Wilaya kuwa na hadhi ya makao makuu kama ilivyo kwa makao makuu mengine ya wilaya, Mwenyekiti amesisitiza kuwa wananchi wa Loliondo na Wilaya yote ya Ngorongoro wamefurahishwa na jambo hilo, lakini pia amesema sio tu suala la Barabara ipo miradi mingi inayotekelezwa katika wilaya ya Ngorongoro ambapo Mhe Rais aipatia fedha nyingi ikiwemo miradi ya Elimu, afya, maji, barabara za vijijini, nk ambapo amesema wananchi wameipokea na kumpongeza Mhe Rais
Mwenyekiti amesema pamoja na Barabara ya WASSO-LOLIONDO km 10 lakini RC Mongela pia aligusia Barabara ya Loliondo-Mtowambu ambapo amesema serikali ipo katika hatua ya kutafuta fedha kwaajili ya kuendeleza matengenezo ya kiwango cha Lami kutoka Sale Juction hadi Mtowambu km 164 zilizobaki ambapo amsema itaendelea kutengenezwa kwa awamu kadiri fedha zitakavyopatikana
Kwa upande wa miradi ya maji Mwenyekiti wa Halmashauri amesema kupitia kikao cha RCC serikali imesema lengo ni kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama katika Maeneo yao vya vijijini, ambapo kikao kimeweka mikakati ya kuisukuma serikali kutoa fedha ili kukamilisha miradi ya maji ambavyo ni viporo na pia miradi mingine isiyo ya maji lakini ni viporo
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.