Afisa Elimu wa Mkoa wa Arusha Mwalimu Gift Kyando (pichani) amewataka Maafisa TEHAMA kufanya kazi kwa uadilifu, weledi na kuonesha juhudi katika kutatua changamoto za kimfumo zinazoikabili Sekta ya Elimu ili kufikia malengo ya Serikali ya ufaulu wa asilimia 90 kwa kila Wilaya.
Mwalimu Gift ametoa wito huo katika kikao kazi cha pamoja cha Mafunzo kwa Maafisa TEHAMA wa Jiji na Halmashauri zote za Mkoa wa Arusha kilichofanyika tarehe 06.04.2018 juu ya jinsi ya kutumia na kufanya matengenezo madogo ya mashine za kurudufisha kilichoendeshwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Kikao hicho ni utekelezaji wa agizo la Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo alilolitoa katika kikao cha pamoja cha Wakurugenzi na Maafisa Elimu wa Mkoa wa Arusha.
Moja wa Washiriki wa mafunzo hayo Mwalimu George James kutoka katika Shule ya Sekondari Osinon akifanya mazoezi ya matumizi ya mashine za kurudufisha
Mwalimu Gift alisema mifumo iliyosimikwa ya PREM na BEMIS katika Mamlaka za Serikali za Mitaa inategemea juhudi na utashi wa Maafisa TEHAMA ili iweze kufanya kazi bila changamoto zozote, aliwasisitiza Maafisa TEHAMA kufanya kazi kwa kushirikiana na Maafisa Elimu hasa katika zoezi linaloendelea la kukusanya taarifa na takwimu za Elimu katika Mfumo wa BEMIS.
Mwalimu Gift Amezitaka Halmashauri zote za Mkoa wa Arusha kukamilisha kazi hiyo kwa wakati bila kusubiri muda wa mwisho ambao husababisha kufanya kazi zisizokuwa na kiwango.
Mhandisi Rexford Pascal akisisitiza jambo katika mafunzo
mafunzo hayo yalitolewa na Bwana Rexford Pascal kutoka katika kampuni ya BMTL Kwa mfano wa mashine ya kurudufisha aina ya RISO yenye uwezo mkubwa wa kurudufisha idadi kubwa ya nakala kwa muda mfupi.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.