Katibu Tawala Wilaya ya Ngorongoro Ndugu Nyakia Ally akiambatana na Mkuu wa Takukuru Wilaya Ndugu Cairo Mwafula leo tarehe 26 Julai 2023 amefanya kikao na watumishi wa Tarafa ya Sale kwa lengo la kukumbusha wajibu na majukumu yao kama watumishi wa umma. Miongoni mwa mambo aliyo wakumbusha watumishi hao ni pamoja na nidhamu na maadali kwa watumishi wa Umma, kutimiza wajibu na majukumu yao kwa mujibu wa sheria Taratibu na Kanuni za Utumishi wa Umma ikiwemo kusimamia ipasavyo miradi ya maendeleo na ikamilike kwa wakati ili iweze kuleta matokeo. yaliokusudiwa. Pia amewakumbusha wajibu wa kukusanya mapato ya Serikali kwenye maeneo yao ikiwemo kubuni vyanzo vipya ya kukusanya mapato ya halmashauri.
Naye Ndugu Cairo Mwafula ametoa elimu kuhusu suala la rushwa na kuwasisitiza jukumu kubwa la Takukuru ni ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za serikali. Ametoa rai kwa Watumishi wa ngazi ya kijiji na Kata, kusimamia vizuri mapato na matumizi ya fedha za serikali pamoja na miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.