Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mhe.Raymond Stephen Mwangwala amewaagiza maafisa elimu kata kushirikiana na viongozi Wa vijiji,kata na wazazi kuthibiti hali ya utoro ili kuhakikisha watoto wote waliojiandikisha wanafanya mitihani ya taifa bila kukosa.
Ameyaeleza hayo leo tar 20/7/2023 katika kikao cha tathmini ya elimu wilayani ngorongoro kilichofanyika katika shule ya loliondo sekondari kikihusisha maafisa elimu wilaya msingi na secondary, katibu tarafa,mwenyekiti wa kamati ya elimu afya na maji,wadhibiti ubora wa elimu,maafisa elimu kata na walimu wakuu kutoka shule zote wilayani hapa.
Mhe.Mwangwala amesifu juhudi zilizofanikisha kufanya vizuri kwa shule nyingi za sekondari wilayani hapa ingawa anataja utoro kama kikwazo kwani matharani kesi nne zimekwisha tolewa hukumu kwa wahalifu waliokua wamewaoa wanafunzi hivyo amewataka walimu kufuata sheria,kanuni,taratibu na miongozo inayotolewa na ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) katika kufumdisha kwani serikali imefanya maboresho mengi ikiwemo miundombinu,vifaa vya kufundishia,ruzuku ya chakula kwa wanafumzi na mengineyo hivyo hakuna kisingizio cha kufanya wanafunzi wasipate elimu bora.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa halmashuri ya wilayani ya Ngorongoro Bw.Nasoro Shemzigwa amewataka walimu wakuu kusimamia nidhamu kwa walimu na wanafunzi sambamba na kufuata ngazi katika mawasiliano,majukumu,kufanya Kazi kama timu,kuacha tabia ya kukaimisha madaraka kuliko kithiri na bila kufuata taratibu,kufuata ngazi katika kuwasiliana na kisimamia sheria,kanuni pamoja na taratibu,huku akiwaomba ushirikiano kwani ni mara ya kwanza kweke kukutana nao tangu awe mkurugenzi wa halmashauri ya ngorongoro na kuahidi atakua nao bega kwa bega katika kutekeleza majukumu yao.
Kwa mujibu wa matokeo ya kidato cha sita 2023 yaliyotangazwa na baraza la taifa la mitihani NECTA kwa shule zilizoko wilayani hapa matokeo yanaonyesha shule zimepata ufaulu wa kuanzia daraja la kwanza hadi la tatu pekee hakuna daraja la nne wala sifuri ambapo shule ya embarway imeongoza ikiwa na daja la kwanza 120 daraja la pili 43 wanafuata Digodigo sekondari daraja la kwanza 37 la pili 12 wakifuatiwa na shule za Nainokanoka,Loliondo,Samunge na Malambo.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.