Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro ,Mhe.Raymond Mwangwala amejumuika kwa pamoja na Waumini mbalimbali wa dini ya kiislamu kupata IFTAR iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji Dkt Jumaa Mhina, katika IFTAR iliyojumuisha Wananchi kutoka sehemu Mbalimbali wakiwemo Viongozi wa Kisiasa , Dini na Watumishi wa serikali na Taasisi mbalimbali za binafsi. Wakati akiongea na Wageni waliohudhuria IFTAR hiyo Mkuu wa Wilaya ,Mhe.Raymond Mwangwala amewataka Wageni hao kuendelea kumwombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt .Samia Suluhu Hassan aendelee kuwa na Afya Njema na nguvu katika kuwatumikia Watanzania pia akazikumbushia jamii katika kusimamia malezi Bora kwa Watoto na kuacha kabisa unyanyasaji wa Kijinsia kwa Watoto ambao ni Taifa la kesho
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.