Mkuu wa wilaya ya ngorongoro Mhe.Raymond Stephen Mwangwala amewaagiza viongozi katika ngazi zote wilayani hapa kupanga mipango ya maendeleo kwa kuzingatia idadi halisi ya watu kwenye maeneo yao .
Maagizo hayo ameyatoa Leo tar 21 April 2023 wakati akizungumza na wananchi kupitia kipindi maalum kilichoandaliwa na Redio ya kijamii ya Loliondo FM kilichoangazia matokeo ya SENSA ya watu na makazi ya 2022 na maadhimisho ya miaka 59 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ambapo mbali na hayo amezungumzia hali ya ulizi na usalama,utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na kutoa salam za Eid al-fitr.
Mhe Mwangwala amesema matokea ya sensa yanaonyesha wilaya ya ngorongoro ina watu 273,449 kati yao wanaume ni 127,850 na wanawake ni 145,699 kati ya hao watu 103,799 wako tarafa ya loliondo,100,793 wako ngorongoro na 68,957 wanaishi tarafa ya sale,kwa upande wa kata kata ya soitsambu inaongoza kwa kua na idadi kubwa ya watu ikiwa na takriban watu 16,899 na kata ya Eyasi ndio yenye idadi ndogo zaidi ikiwa na watu 2,800 huku wilaya ikiwa na makaazi 60,883.
Katika hatua nyingine mkuu wa wilaya amewataka wananchi kushiriki kutunza mazingira kwa kupanda miti katika maeneo yao ili kukabiliana na ukame unaotishia maisha ya mifugo na mazao kwa wafugaji na wakulima ambao ndio idadi kubwa ya wananchi wa ngorongoro pia amewasihi wananchi kufanya usafi kuanzia maeneo ya makazi hadi ya biashara ili kudumiaha usafi na kuendelea kuenzi muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fenda nyingi kwaajili ya miradi ya afya,elimi,miundombinu ya barabara kupitia TARURA,Afya,elimu na kadhalika,huku akiwataka wakandarasi wanaotekeleza miradi hiyo kuikamilisha kwa wakati na viwango stahiki kwani hali ya ulinzi na usalama kiwilaya ni shwari ambayo mbali na wao inawaruhusu pia wananchi kuendelea na shughuli za kimaendeleo bila woga wala hofu.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.